Serikali imeshauliwa kupunguza idadi ya kodi inazowatoza wakulima na wafanyabiashara katika biashara moja ili kupunguza ukwepaji
kodi miongoni mwao.
Akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na taasisi ya EABMTI
mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara mkoani (TCCIA) Iringa Nd Lukasi
Mwakabungu amesema kodi hizo zimekua kero kwa wakulima na hivyo kuwafanya
washindwe kuendesha kilimo chenye tija kwani muda mwingi wamekua wakiutumia
kukwepa kodi badala ya kuzalisha.
Bw Mwakabungu ameitaka serikali kujenga viwanda vidogo vya
usindaikaji ili kuweza kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha wakulima hapa
nchini na kukuza mnyororo wa thamani.
Mdahalo huo umewahusisha wakulima na wafanyabiashara wa mkoa
wa Iringa ili kuhamisasha wananchi wachague viongozi watakaoijenga Tanzania
tunayoitaka.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment