Tanzania imechaguliwa
kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Watalaam wa Fedha,Uchumi na Mipango kwa nchi
wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) na Kamisheni ya Uchumi ya Afrika (ECA) kwa
kipindi cha mwaka mmoja.
Uchaguzi huo
ulifanyika baada ya ufunguzi wa kikao cha Kamati ya watalaam wa Fedha,Uchumi na
Mipango ambacho kinaendelea Mjini Addis Ababa –Ethiopia. Kabla ya uteuzi huo
nafasi hiyo ya Mwenyekiti ilikuwa inashikiliwa na Nigeria.
Ukanda
wa nchi za Mashariki mwa Afrika ulipewa nafasi ya kuwa mwenyekiti na wajumbe wa
nchi kutoka ukanda huo kwa pamoja waliichagua wajumbe hao waliipa
Tanzania heshima hiyo. Nchi zilizoipigia kura Tanzania kuwa Mwenyekiti ni Ethiopia, Eritrea, Madagascar, Kenya,
Uganda, Burundi, Rwanda,Sudan Kusini, Djibout, Somalia, Msumbiji, Comoro,
Mauritius na Seychelles.
Pamoja na Tanzania
kuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo,pia Misri ilichaguliwa kuwa Makamu wa kwanza wa
Mwenyekiti ikiwakilisha nchi za Kaskazini mwa Afrika,Gabon kuwa Makamu wa pili
wa Mwenyekiti ikiwakilisha nchi za Afrika ya kati,Afrika ya Kusini Makamu wa
tatu wa Mwenyekiti ikiwakilisha nchi za Kusini mwa Afrika na Guinea
ilichaguliwa kuwa Katibu ikiwakilisha nchi za Afrika Magharibi.
0 comments:
Post a Comment