Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » »

Hizi ndio rekodi 7 za Cristiano Ronaldo alizoweka mwaka 2015 pekee …

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuweka rekodi kadhaa kubwa katika soka, ukiachana na kutwaa tuzo ya tatu ya mchezaji bora wa Dunia  Ballon d’Or kwa mwaka 2015, Ronaldo amefanikiwa kuweka rekodi 7 mpya.
7- Ronaldo amefanikiwa kufunga jumla ya hat-trick 28 katika kipindi cha mwaka 2009-2015, toka amejiunga na Real Madrid mwaka 2009 hadi 2015, Ronaldo anakuwa mchezaji anayeongoza kwa ufungaji wa hat-trick nyingi katika historia ya Laliga.
6- Kufunga magoli 48 kwa msimu mmoja akiwa na Real Madrid. Ronaldo alifunga jumla ya magoli 48 katika msimu wa 2014/2015 na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli mengi katika msimu ndani ya Real Madrid.
Ronaldo-Shot
5- Kufunga magoli 50 kwa misimu mitano mfululizo. Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza Hispania kufunga magoli 50 katika misimu mitano mfululizo, alianza kufanya hivyo mwaka (2010/11–2014/15).
4- Kufunga magoli 61 kwa msimu mmoja katika mashindano yote aliyocheza ndani ya msimu wa mwaka 2014/2015.
3- Kuvunja rekodi ya ufungaji wa goli 323 ya mkongwe wa Real Madrid Raul. Ronaldo amefunga jumla ya 338 hadi sasa katika michezo 325 ndani ya  Real Madrid, wakati Raul aliweka rekodi ya kufunga goli 323 kwa kucheza michezo 741.
Raul-5
2- Kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli 11 katika michuano ya klabu Bingwa Ulaya hatua za makundi kwa msimu wa 2015/2016.
1- Kuwa mchezaji pekee kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa Ulaya mara nne kwa kufunga jumla ya goli 48 kwa msimu wa 2014/2015.
MADRID, SPAIN - NOVEMBER 05: Cristiano Ronaldo of Real Madrid CF kisses his Golden Boot 2014 award at Melia Castilla hotel on November 5, 2014 in Madrid, Spain. Cristiano Ronaldo,s 31 strikes in La Liga last season have given him his third Golden Boot award. This year he has shared the award with FC Barcelona player Luis Suarez for the best scorer in Europe. Both players have scored the same number of goals thorough 2013-2014 season. (Photo by Gonzalo Arroyo Moreno/Getty Images)
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.