Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » » WATENDAJI WASIMAMIE KIUKAMILIFU ULINZI NA USALAMA

WATENDAJI WASIMAMIE KIUKAMILIFU ULINZI NA USALAMA

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Juma Masenza amewataka watendaji wa kata kuhakikisha wanasimamia kikamilifu suala la ulinzi na usalama katika kata wanazoziongoza, kwa kuzingatia kuwa hilo ni moja kati ya majumu yao makubwa katika kata zao.


Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya habari na mawasiliano ya halmasha ya wilaya ya Mufindi imeeleza kuwa, Mkuuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo wakati wa kikao  maalum na watendaji wa kata 30 za halmashauri ya wilaya mufindi kilichofanyika mjini Mafinga.

Bi. Masenza amesema, jukumu la kusimamia maisha na mali za wananchi katika kata wanazoziongoza ni jukumu la msingi kwa ustawi wa maisha ya watu na taifa kwa ujumla hivyo, linapaswa kupewa kipaumbele

Aidha mkuu huyo wa Mkoa amewahimiza watendaji hao kujibidisha ili waweze kubaini mipango ya uvunjaji wa amani na usalama kabla haijatekelezwa kuliko kushughulikia baada ya kufanyika kwa uhalifu hususani unaosababisha vifo kwa raiya jambo ambalo linakuwa halina maana kwa umma

Awali akitoa mada  kuhusu majukumu ya watendaji wa kata, katibu tawala msaidizi wa serikali za mitaa Mkoa wa Iringa Bw.Wilfred Myuyu, pamoja na mambo mengine amewataka baadhi ya watendaji wa kata kuacha tabia zinazo dhalilisha utumishi wa umma zikiwemo za ulevi, uwizi, kutoa siri za serikali sanjari na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji kazi badala ya kujifanya miungu watu katika maeneo yao ya kazi.


Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.