Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » » SERIKALI YA TAKIWA KUPUNGUZA IDADI YA KODI KWA MAZAO YA WAKULIMA

SERIKALI YA TAKIWA KUPUNGUZA IDADI YA KODI KWA MAZAO YA WAKULIMA




Serikali imeshauliwa kupunguza idadi ya kodi  inazowatoza  wakulima na wafanyabiashara  katika biashara moja ili kupunguza ukwepaji kodi miongoni mwao.

Akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na taasisi ya EABMTI mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara mkoani (TCCIA) Iringa Nd Lukasi Mwakabungu amesema kodi hizo zimekua kero kwa wakulima na hivyo kuwafanya washindwe kuendesha kilimo chenye tija kwani muda mwingi wamekua wakiutumia kukwepa kodi badala ya kuzalisha.





Bw Mwakabungu ameitaka serikali kujenga viwanda vidogo vya usindaikaji ili kuweza kuongeza thamani ya mazao wanayozalisha wakulima hapa nchini na kukuza mnyororo wa thamani.

Mdahalo huo umewahusisha wakulima na wafanyabiashara wa mkoa wa Iringa ili kuhamisasha wananchi wachague viongozi watakaoijenga Tanzania tunayoitaka.

MWISHO
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.