Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » » Takriban mateka 147 wauawa katika Chuo kikuu cha Garissa

Takriban mateka 147 wauawa katika Chuo kikuu cha Garissa

Serikali ya Kenya imetangaza kwamba zaidi ya mateka 147 waliokua wakishikiliwa tangu Alhamisi asubuhi wiki hii katika Chuo kikuu cha Garissa, mshariki mwa Kenya, wameuawa.

Serikali ya Kenya imefahamisha pia kwamba watekaji nyara wanne wameuawa na vikosi vya usalama. Katika shambulio hilo watu zaidi ya 80 wamejeruhiwa.
Awali, waziri wa mambo ya ndani, Joseph Nkaiserry, alisema kuwa watu 15 waliuawa na wengine zaidi ya 50 walijeruhiwa katika shambulio lililoendeshwa na watu wenye silaha katika Chuo kuu cha Garissa, Mashariki mwa Kenya, kilomita 150 na mpaka wa Somalia.
Serikali ya Kenya imemtaja Mohammed Kuno ambaye anajulikana kwa jina la Gama Adhere kama mshukiwa aliyepanga shambulio hilo, ambalo limegharimu mpaka sasa maisha ya watu 147.
Serikali ya Kenya imetoa zawadi nono ya dola 53,000 kwa atakayemkamata Mohammed Kuno au atakayetoa taarifa kuhusu mshukiwa huyo.
Wakati huohuo Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ametuma risala za rambi rambi kwa familia za watu waliouawa katika shambulio lililotokea katika chuo kikuu cha Garissa mashariki mwa Kenya.Rais Uhuru Kenyatta pia amewahakikishia raia wa Kenya kuwa serikali yake imechukua hatua ya kuongeza vikosi vya usalama katika eneo hilo.
Rais Kenyatta amewatolea wito raia wa Kenya kuwa watulivu, wakati vikosi vya usalama vikiendelea na operesheni ya kuwaska washambuliaji.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya, shambulio hilo lilianza saa za swala mapema asubuhi, kwenye majira ya saa kumi na moja na nusu leo Alhamisi. Idadi ya watu walioendesha shambulio hilo haijajulikana
Kwa mujibu wa gazeti la Kenya la The Standard, wanafunzi waliofaulu kuondoka chuoni hapo, wamesema waliwaona watu watano wenye silaha.
Kwa mujibu wa polisi ya Kenya, watu hao wenye silaha, walianza kufyatua risase walipoingia chuoni hapo.
Kundi la Al Shabab limekiri kutekeleza shambulio hilo. Kwa mujibu wa mashahidi, wakati watu wenye silaha walipoingia katika Chuo kikuu hicho walikua wakiwatenganisha wanafunzi kufuatia imani zao, huku wakristo wakiuawa.
Hili ni shambulio baya kuwahi kutokea katika ardhi ya Kenya tangu shambulio dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Nairobi mwaka 1998.
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.