Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » » Rais Zuma awatembelea waathirika wa ghasia

Rais Zuma awatembelea waathirika wa ghasia

Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini amewaomba raia wa kigeni kubakia nchini humo wakati wakati akikatisha ziara yake ya kiserikali nchini Indonesia kushughulikia wimbi hilo la chuki dhidi ya wageni. Wiki tatu za ghasia zinazoongezeka dhidi ya wageni nchini Afrika kusini zimesababisha kiasi watu sita kuuwawa na kuwalazimisha wahamiaji 5,000 kutafuta hifadhi katika makambi ya muda.

Machafuko hayo , ambayo yameanzia katika mji wa mashariki wa bandari wa Durban kabla ya kusambaa katika maeneo mengine ya nchi hiyo, yanabeba ghasia za hisia za chuki dhidi ya wageni ambazo ziliikumba Afrika kusini mwaka 2008 wakati watu 62 walipouawa.

Katika tukio la hivi karibuni kabisa, polisi jana Jumamosi(18.04.2015) wamesema wageni waliouwawa wamefariki kutokana na kuchomwa visu mjini Alexandra , mji ulioko kaskazini mwa Johannesburg. Eneo hilo linaloishi watu masikini limekuwa lengo ya ghasia nyingi katika siku hiyo, ambapo maafisa wa polisi walifyatua risasi za mipira kuwatawanya watu waliokuwa wakifanya uporaji.

Zaidi ya watu 30 wamekamatwa usiku ya Jumamosi kuzunguka mji wa Johannesburg pekee. Akiwa chini ya mbinyo kuzuwia kurudiwa mauaji yaliyotokea mwaka 2008, Zuma alisafiri kwenda Durban kutembelea kambi wanayohifadhiwa wageni waliokimbia makaazi yao kutokana na ghasia hizo, lakini alikabiliana na mapokezi yasiyokuwa mazuri kutoka kwa kundi lililomsubiri, ambalo lilipaaza sauti, "rudi nyumbani, rudi nyumbani" na umechelewa , umechelewa".

"Kama serikali , hatuwaambii nendeni zenu". Sio kila raia wa Afrika kusini anasema , nendeni zenu". Ni idadi ndogo sana ya watu ambao wanasema hivyo," Zuma amesema katika kambi ya Chatsworth, ambako alikabidhi hundi ya dola 4,100 kuwasaidia wahanga wa ghasia za chuki dhidi ya wageni.

Ameahidi kumaliza ghasia hizo na alilihakikishia kundi hilo la watu kwamba kuna nafasi kwa wageni nchini Afrika kusini. "Hata kama kuna wale wanaotaka kurejea nyumbani, wafahamu kwamba wakati tutakapositisha ghasia wanakaribishwa kurejea, " Zuma amesema.


Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.