Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » » Watu 140 wauawa Yemen katika vita vilivyopamba moto

Watu 140 wauawa Yemen katika vita vilivyopamba moto


Mapigano makali kati ya waasi wa Houthi na wapiganaji watiifu kwa utawala wa Yemen yamesababisha vifo vya watu 140 huku shirika la msalaba mwekundu likishindwa kufikisha misaada ya kibinadamu kwa waathiriwa.


Wafanyakazi wa kutoa misaada wameonya kuwa hali inazidi kuwa mbaya katika taifa hilo masikini la kiarabu ambako Saudi Arabia na washirika wake wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kijeshi ya angani kwa siku kumi na tatu sasa dhidi ya waasi wa Houthi.

Maafisa nchini humo wamesema mapigano makali yameripotiwa katika mji wa kusini mwa nchi hiyo wa Aden anakotoka Rais wa Yemen Abderabbo Mansour Hadi ambaye ametorokea Saudi Arabia.
Watu 53 ambao ni thuluthi moja ya waliouawa katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita, waliuawa wakati waasi wa Houthi walipojaribu kuidhibiti bandari moja mjini Aden.

Waasi 19 wa Houthi na wapiganaji 15 wa makundi ya wapiganaji wanaomuunga mkono Hadi wameuawa usiku wa kuamkia leo katika mji wa Daleh kaskazini mwa Adeb na watu wengine saba wameuawa katika jimbo la kusini mwa Yemen la Abyan.

Mji wa Aden waathirika zaidi
Wapiganaji wanaomuunga mkono Hadi wanaidhibiti kambi ya Abyan ya kikosi cha wanajeshi walio watiifu kwa Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh anayeshutumiwa kuwaunga mkono waasi wa Houthi.

Hadi ambaye anatambuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa kiongozi halali wa Yemen, alitorokea Aden mwezi Februari baada ya wahouthi kuuteka mji mkuu Sanaa na kuchukua madaraka.

Baadaye mwezi uliopita alikimbilia Saudi Arabia baada ya waasi hao kuanza kuusogelea mji wa Aden na kuichochea Saudi Arabia na nchi nyingine za kisunni kuanzisha kampeini ya kijeshi dhidi ya waasi hao.
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.