Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini amewaomba raia wa kigeni kubakia nchini
humo wakati wakati akikatisha ziara yake ya kiserikali nchini Indonesia
kushughulikia wimbi hilo la chuki dhidi ya wageni.
Wiki tatu za ghasia zinazoongezeka dhidi ya wageni nchini Afrika kusini
zimesababisha kiasi watu sita kuuwawa na kuwalazimisha wahamiaji 5,000
kutafuta hifadhi katika makambi ya muda.
Machafuko hayo , ambayo yameanzia katika mji wa mashariki wa bandari wa
Durban kabla ya kusambaa katika maeneo mengine ya nchi hiyo, yanabeba
ghasia za hisia za chuki dhidi ya wageni ambazo ziliikumba Afrika kusini
mwaka 2008 wakati watu 62 walipouawa.
Katika tukio la hivi karibuni kabisa, polisi jana Jumamosi(18.04.2015)
wamesema wageni waliouwawa wamefariki kutokana na kuchomwa visu mjini
Alexandra , mji ulioko kaskazini mwa Johannesburg. Eneo hilo linaloishi
watu masikini limekuwa lengo ya ghasia nyingi katika siku hiyo, ambapo
maafisa wa polisi walifyatua risasi za mipira kuwatawanya watu waliokuwa
wakifanya uporaji.
Zaidi ya watu 30 wamekamatwa usiku ya Jumamosi kuzunguka mji wa
Johannesburg pekee. Akiwa chini ya mbinyo kuzuwia kurudiwa mauaji
yaliyotokea mwaka 2008, Zuma alisafiri kwenda Durban kutembelea kambi
wanayohifadhiwa wageni waliokimbia makaazi yao kutokana na ghasia hizo,
lakini alikabiliana na mapokezi yasiyokuwa mazuri kutoka kwa kundi
lililomsubiri, ambalo lilipaaza sauti, "rudi nyumbani, rudi nyumbani" na
umechelewa , umechelewa".
"Kama serikali , hatuwaambii nendeni zenu". Sio kila raia wa Afrika
kusini anasema , nendeni zenu". Ni idadi ndogo sana ya watu ambao
wanasema hivyo," Zuma amesema katika kambi ya Chatsworth, ambako
alikabidhi hundi ya dola 4,100 kuwasaidia wahanga wa ghasia za chuki
dhidi ya wageni.
Ameahidi kumaliza ghasia hizo na alilihakikishia kundi hilo la watu
kwamba kuna nafasi kwa wageni nchini Afrika kusini. "Hata kama kuna wale
wanaotaka kurejea nyumbani, wafahamu kwamba wakati tutakapositisha
ghasia wanakaribishwa kurejea, " Zuma amesema.
Home »
» Rais Zuma awatembelea waathirika wa ghasia
Rais Zuma awatembelea waathirika wa ghasia
Posted by COUNTRYFM IRINGA
Posted on 12:17 AM
with No comments
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula
0 comments:
Post a Comment