Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » »

Mchezaji aliyemtongoza mwanahabari aadhibiwa


Nahodha wa zamani wa timu ya kriketi ya West Indies, Chris Gayle amepigwa faini baada yake kumtongoza mwanahabari wakati wa mahojiano ya moja kwa moja. Gayle amepigwa faini ya dola 10,000 za Australia (sawa na $7,200; £4,900) na klabu yake ya Melbourne Renegades inayocheza ligi ya Big Bash.
Mchezaji huyo alimuuliza mwanahabari wa kipindi cha Ten Sport Bi Mel McLaughlin kama wangeweza kwenda ‘date’ alipokuwa akihojiwa wakati wa mechi ya ligi dhidi ya Hobart Hurricanes Jumatatu. “Kuyatazama macho yako mara ya kwanza kabisa ni jambo njema sana. Natumai tunaweza kuketi na kunywa kinywaji pamoja. Usione haya mtoto,” alimwambia.
Baadaye, amejitetea na kusema alikuwa tu anafanya mzaha. Chris Rogers, aliyekuwa nahodha wa Sydney Thunder wakati Gayle alikuwa mchezaji wa kawaida ameambia shirika la habari la ABC Grandstand kwamba hajashangazwa na kitendo hicho cha Gayle.
Gayle
Gayle, 36, ni mzaliwa wa Jamaica lakini huchezea West Indies
Klabu ya Melbourne Renegades imesema matamshi hayo yalikuwa hayafai kabisa na yalikuwa ya “kuvunja heshima”. Maafisa wa klabu hiyo wameomba radhi kwa McLaughlin na umma pia.
Pesa kutoka kwa faini aliyotozwa mchezaji huyo zitakjabidhiwa wakfu wa McGrath unaosaidia watu wanaotatizwa na saratani ya matiti.
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.