Posted by COUNTRYFM IRINGA
Posted on 12:42 AM
with No comments
Aidha, kimesema suluhisho la hali ya sasa ya Zanzibar ni vyama
vingine vyote, kujumuishwa katika mazungumzo baina ya vyama vya CCM na
CUF ili kupata mawazo jumuishi na yatakayowakilisha sehemu kubwa zaidi
ya Wazanzibari ambao wengi wao, hasa kizazi kipya, hawana uhusiano
wowote na vyama hivyo viwili.
Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto
baada ya kikao cha Kamati ya Uongozi iliyokutana Zanzibar mwishoni mwa
wiki.
Kwa mujibu wa Zitto, ACT-Wazalendo inasikitishwa na hali ngumu ya
maisha inayowakumba wananchi wa Zanzibar kutokana na mkwamo wa kisiasa
unaoendelea visiwani humo.
Kutokana na hali hiyo, ACT-Wazalendo imependekeza kwa ajili ya
mustakabali mwema wa Zanzibar, mazungumzo yoyote kuhusu uchaguzi
uliofutwa yahusishe wadau wa vyama na taasisi nyingine walioshiriki
kwenye uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment