Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » » Netanyahu alionya bunge la Marekani kuhusu Iran

Netanyahu alionya bunge la Marekani kuhusu Iran

Waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu amelionya bunge la Marekani kwamba mkataba na Iran uliopendekezwa hautazuia wala kupunguza uwezo wake wa kutengeneza mabomu ya nyuklia. 

Akilihutubia bunge hilo hapo jana Netanyahu alizikosoa juhudi za rais wa nchi hiyo Barack Obama kutafuta makubaliano na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia wenye utata. Netanyahu ameonya kwamba utawala wa Obama unaifungulia mlango Iran kuelekea kutengeneza bomu la nyuklia. 

Obama hakuitazama hotuba ya Netanyahu kwa kuwa alikuwa akizungumza na viongozi wa Ulaya kuhusu mzozo unaoendelea nchini Ukraine. Akizungumza baada ya hotuba hiyo rais Obama alisisitiza kwamba Netanyahu hana mpango wowote wa kukabiliana na kitisho cha Iran na hakusema lolote jipya katika hotuba yake.

Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.