Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » » AFISA MTENDAJI AUWAWA

AFISA MTENDAJI AUWAWA









Mtendaji wa Kijiji cha Mpona Kata ya Totowe Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Bahati Yaledi Mwanguku(38) ameuwa  na majambazi wawili waliokuwa na mapanga kisha kuporwa pikipiki na simu na simu yake ya mkononi akiwa nyumbani kwake alfajiri Machi 3,mwaka huu.

Marehemu alikuwa nyumbani ambapo wauaji hao walifika nyumbani kwa Mtendaji wakimtaka awafungulie kwa madai kuwa n'gombe wao wameporwa na majambazi katika eneo lake hivyo wanaomba msaada wake waio wakiwa wametokea Mbarali.

Hata hivyo Mtendaji hakujibu chochote ambapo Vijana wawili kazi Juhudi Mwanda(19) na Huruma Simfukwe(34) waliokuwa wanaishi na Mtendaji ambao walilala nyumba ya nje waliwataka Majambazi kutomwamsha Mtndaji kwa vile alipumzika hivyo waje asubuhi ili watatuliwe tatizo lao.


Majambazi hayo yalikataa na kusisitiza Mtendaji aamke ndipo Marehemu alijibu na kuwataka Majambazi hayo yamuone Mgambo anayeitwa Tatizo ili waende eneo la tukio lakini walikataa wakidai Tatizo ndiye aliyewaamuru waje kwake.

Baada ya mabishano ya muda wa dakika 15 Majambazi hayo yalimkamata Huruma Simfukwe na kumfunika kwa shuka usoni kisha kufungua mlango wa nyumba aliyokuwa amelala Mtendaji na kumfunika kwenye uvungu wa kochi lililokuwa sebuleni na kuanza kumcharanga Bahati Mwanguku kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na kupoteza maisha papo hapo.

Mara baada ya kutekeleza mauaji hayo majambazi hayo yalichukua pikipiki ya Mtendaji iliyokuwa imefungwa kisha kuondoka nayo kwa kuikokota hadi barabarani ambapo walifanikiwa kuiwasha wakielekea njia ya Namkukwe.

Wakati wa tukio hilo mke wa Mtendaji aliyefahamika kwa jina la Grace Shughuli(37)alikuwa amesafiri muda mfupi ndipo mumewe alikumbwa na mauti na binti yake mkubwa Irene Bahati(16)anayesomba shule ya sekondari ya Totowe alifanikiwa kutoroka na kuwaamsha majirani ambao walifika eneo la tukio na kukuta chumba kimetapakaa damu iliyotokana na majeraha makubwa.

Baadhi ya wananchi walifanya juhudi za kuwafuatili majambazi hayo hadi eneo la Maonwa Kata ya Namkukwe lakini hawakuweza kufanikiwa kuwapata wahalifu hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpona Pugu Saida Ngolope alitoa taarifa kwa Mtendaji Kata Ronward Mwashiuya lakini hakuwepo nyumbani kwake alikuwa Mbeya kikazi na kwamba Mwashiuya alimtaka Mwenekiti kutoa taarifa Polisi kituo cha Galula na kwa Diwani wa Totowe Godian Wangala.

Polisi walifika eneo la tukio  majira ya asbuhi na kuanza uchunguzi wa awali ili kuwabaini wahusika wa tukio hilo la kinyama ambapo wakishirikiana na madaktari baada ya uchunguzi mwili ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Mtendaji Kata Ronward Mwashiuya alitoa taarifa kwa Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro  ambaye na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Sophia Kumbuli ambaye ni Mwajiri wa Watumishi wa Halmashauri.

Kumbuli amelaani vikali tukio hilo la kinyama na kusema kuwa watumishi wengi wapo vijijini hivyo watafanya kazi kwa hofu wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku na wengi wao wapo vijijini hivyo ametaka wananchi wa Wilaya ya Chunya kusaidia kuwapa ulinzi watumishi wa kada mbali mbali ili kusukuma maendeleo katika maeneo yao.

Baadhi ya watumishi mbali mbali waliofika eneo la tukio na Diwani wa Kata ya Namkukwe Conrad Mkondya wameliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi ili  kuwabaini wahusika na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika pia kuimarishwa kwa Daftari la wageni wanaoingia katika maeneo yao kwani wahalifu wengi wamefanya bande hilo kama maficho ya uhalifu.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Jeshi lake limeanza uchunguzi wa na kuomba wananchi watoe ushirikiano ili kuwapata wahalifu ili wachukuliwe hatua za kisheria na kutumia fursa hii kuwaomba wananchi kuharakisha ujenzi wa kituo cha Polisi Kata ya Totowe ili kuimarisha ulinzi zaidi.

Matukio ya ujambazi katika Kata ta Namkukwe na Totowe yamekuwa yakitokea mara kwa mara hasa katika msimu wa kilimo na mavuno na njia hiyo kutumia kuingia na kutoka kupitia wilaya ya Momba na Mbozi na wadau wameomba viongozi wa wilaya hizo kukutana ili kukomesha vitendo vya uhalifu
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.