Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya

.

.

.
  • Home
  • SIASA NA UCHUMI
  • MICHEZO
  • MUZIKI
  • HABARI
  • MAZINGIRA
  • LEO KATIKA HISTORIA
  • KILIMO
Home » »

Posted by COUNTRYFM IRINGA Posted on 1:30 AM with No comments
                             MABASI YAENDAYO KASI
MAWAZIRI wawili jana ‘walitumbua majipu’ baada ya kutangaza kusimamishwa kazi kwa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), Asteria Mlambo na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Diwani Msemo, wote wakipisha uchunguzi dhidi yao.Mlambo amesimamishwa kazi kuanzia jana ili kupisha uchunguzi baada ya serikali kubaini ukiukwaji wa wazi wa Sheria ya Manunuzi ya Umma katika kumpata mtoa huduma ya mpito wa mradi huo wenye nia ya kupunguza msongamano wa magari barabarani kwa madhumuni ya kurahisisha usafiri na usafirishaji jijini Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene alisema kutokana na kukamilika kwa sehemu ya ujenzi wa miundombinu ya Awamu ya Kwanza ya mradi, Serikali iliamua kuwa na mtoa huduma wa mpito kabla ya kumpata wa kudumu.“Mtoa huduma wa mpito alipaswa kupatikana kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma. Hata hivyo, Serikali imebaini ukiukwaji wa wazi wa sheria hiyo wakati wa kumpata mtoa huduma wa kipindi cha mpito.
“Kufuatia hali hiyo nimeamua kumsimamisha kazi kuanzia leo tarehe 23 Desemba, 2015, Mtendaji Mkuu wa DART, Bi. Asteria Mlambo ili kupisha uchunguzi,” alieleza Simbachawene.
Times Fm TZ's photo.

Tweet
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home

SIKILIZA COUNTRY FM

Get the Flash Player to see this player. Shoutcast & Icecast Server

Pages

  • Home

Pages

  • Home
radio country fm,one community. Powered by Blogger.
  • Home

Pageviews

Support : Country Fm | |
Copyright © 2015. . - All Rights Reserved
Template Created by Country Fm Published by Country fm radio
Proudly powered by Blogger