Ifahamu stori iliyomkutanisha D’Banj na Kanye West mpaka kutengenezwa kwa ‘Oliver Twist’!
Kati ya ngoma kubwa za staa wa muziki kutoka Nigeria, D’Banj huwezi kuacha kuitaja hit song ya Oliver Twist… Nimekutana na interview ya D’Banj na jarida la Forbes Africa (December 2015) na kikubwa kilichonigusa ni stori iliyompelekea mpaka kukutana na Kanye West na hatimaye kupata mchongo wa kutengeneza ‘Oliver Twist’ single yake ya kwanza chini ya G.O.O.D Music lebo inayomilikiwa na Kanye West.
D’Banj.
>>> “Kanye
West na mimi tulikutana kwa bahati mbaya… nilikuwa Dubai na crew yangu
tukisubiri kubadilisha ndege, tukiwa tunasubiri wahudumu kadhaa wa
ndege wakaja kwangu kwa spidi huku wakiita ‘Mr Kanye West’… nikashangaa
na kujitazama juu mpaka chini na kisha nikawatazama na waliponikaribia
nikatoa mkono na kuwaambia ‘mambo naitwa D’Banj lakini kama nafanana na
Kanye West basi inamaanisha yupo maeneo haya..’. Tukaanza kumtafuta na
tulipompata tukamuelezea kilichotokea na hapo ndipo kila kitu
kilipoanzia… Nilikutanishwa na Kanye baada ya wahudumu wa ndege
kunifananisha naye...” <<< D’Banj.
Kanye West.
Baada ya D’Banj na Kanye West kukutana Airport, Dubai, wawili hao waliongea mengi na D’Banj akatumia fursa hiyo kumsikilizisha Kanye baadhi ya kazi zake… baada ya rapper huyo wa Marekani kuvutiwa na midundo ya D’Banj mastaa hao wakapeana namba kisha wakaachana…
>>> “Baada
ya kukaa na kuzungumza naye mambo mengi, akaomba tubadilishane namba…
nikampatia yangu akanipatia yake tukaachana. Baada ya wiki kadhaa
akanipigia na kuniomba niende Los Angeles kwa mazungumzo zaidi,
nilipofika huko Kanye akanitambulisha kwa mastaa wenye majina makubwa
kwenye muziki kama Big Sean, Pusha T, Hit-Boy na LA Ried… tukasign
mikataba na siku chache badaaye tukarekodi ‘Oliver Twist’…” <<< D’Banj.
Single ya Oliver Twist ilimpa D’Banj mafanikio makubwa kwenye levo za kimataifa pamoja na kukuza jina lake kwenye nchi kama Uingereza na Marekani… na kwa sasa single ya ‘Oliver Twist’ inagusa watazamaji milion 36, 422, 917 kwenye mtandao wa YouTUBE ikiwa ni moja ya videos za wasanii wa Africa ziliyotazamwa zaidi!
0 comments:
Post a Comment