Vikosi vya usalama vya Burundi vimefyetua risasi na gesi za kutoa
machozi dhidi ya waandamanaji wanaoendelea kuteremka majiani kupinga
muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza.
Katika mji mkuu Bujumbura,
mamia wamepuuzia amri ya serikali na kuteremka majiani, wakimtaka Rais
Nkurunziza aachilie mbali azma yake ya kugombea muhula wa tatu.
Mwanajeshi mmoja ameuwawa hii leo, polisi walipofyetua risasi
kuwatawanya waandamanaji. Kisa hicho kinapalilia mfarakano uliozuka kati
ya vikosi vya polisi na vile vya jeshi.
Uamuzi wa Rais Nkurunziza wa
kuchelewesha uchaguzi wa bunge na ule wa serikali za mitaa hadi Juni
tano ijayo, umekataliwa na upande wa upinzani na kukosolewa na mashirika
ya haki za binaadamu na yale ya kiraia.
Mkuu wa shirika la kiraia,
Vital Nshimirimana, amesema kucheleweshwa kwa chaguzi hizo hakusaidii
kitu kwa sababu suala muhimu, ambalo ni Rais Nkurunziza kuwania muhula
wa tatu, limebakia pale pale.
Naye makamo mwenyekiti wa chama cha
upinzani cha FRODEBU, Frederic BAMVUGINYUMVIRA, anasema hawakuridhishwa
na kuahirishwa huko "kwa sababu matatizo ya Waburundi hayakufumbuliwa."
Home »
» Vikosi vya usalama vyapambana na waandamanaji Burundi
Vikosi vya usalama vyapambana na waandamanaji Burundi
Posted by COUNTRYFM IRINGA
Posted on 10:15 PM
with No comments
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula
0 comments:
Post a Comment