Jeshi la anga la Kenya (KDF) limezishambulia kambi mbili za al Shabaab
nchini Somalia leo hii. Chanzo kutoka katika jeshi hilo kimesema hilo ni
shambulio la kwanza kubwa baada ya shambulizi la wiki iliyopita la
wanamgambo wa kundi hilo katika chuo kikuu cha Kenya.
Ndege za kivita
zilishambulia kambi hizo zilizopo Gondodowe na Ismail, zote zikiwa
katika jimbo la Gedo, lililopo mpakani mwa Somalia na Kenya.
Chanzo
hicho kiliendelea kusema kutanda kwa kiwango kikubwa cha moshi angani
kumefanya iwe vigumu kuweza kutambua athari za mashambulizi katika
maeneo hayo ya kambi.
Aidha afisa huyo wa KDF alisema waliyalenga maeneo
hayo mawili kutokana na kupata taarifa kuwa wafuasi wa al-Shabaab
wanaoishambulia Kenya wanatokea katika kambi kambi hizo. Afisa huyo wa
jeshi aliyesamema hayo akitolea mfano shambulizi lililosababisha mauwaji
makubwa katika Chuo Kikuu mjini Garisa, kilichopo umbali wa kilometa
200 kutoka mpakani mwa Somalia.
Home »
» Kenya yashambulia kambi za al-Shabaab
Kenya yashambulia kambi za al-Shabaab
Posted by COUNTRYFM IRINGA
Posted on 4:19 AM
with No comments
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula
0 comments:
Post a Comment