Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » » Vikosi vya usalama vyapambana na waandamanaji Burundi

Vikosi vya usalama vyapambana na waandamanaji Burundi

Vikosi vya usalama vya Burundi vimefyetua risasi na gesi za kutoa machozi dhidi  ya waandamanaji wanaoendelea kuteremka majiani kupinga muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza.


Katika mji mkuu Bujumbura, mamia wamepuuzia amri ya serikali na kuteremka majiani, wakimtaka Rais Nkurunziza aachilie mbali azma yake ya kugombea muhula wa tatu.

Mwanajeshi mmoja ameuwawa hii leo, polisi walipofyetua risasi kuwatawanya waandamanaji. Kisa hicho kinapalilia mfarakano uliozuka kati ya vikosi vya polisi na vile vya jeshi.

Uamuzi wa Rais Nkurunziza wa kuchelewesha uchaguzi wa bunge na ule wa serikali za mitaa hadi Juni tano ijayo, umekataliwa na upande wa upinzani na kukosolewa na mashirika ya haki za binaadamu na yale ya kiraia.

Mkuu wa shirika la kiraia, Vital Nshimirimana, amesema kucheleweshwa kwa chaguzi hizo hakusaidii kitu kwa sababu suala muhimu, ambalo ni Rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu, limebakia pale pale.

Naye makamo mwenyekiti wa chama cha upinzani cha FRODEBU, Frederic BAMVUGINYUMVIRA, anasema hawakuridhishwa na kuahirishwa huko "kwa sababu matatizo ya Waburundi hayakufumbuliwa."

Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.