Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya

Mwenyekiti Chadema apongeza kasi ya JPM


MWENYEKITI wa Chadema mkoa wa Rukwa, Zeno Nkoswe amepongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutumbua majipu na vijipu. Akizungumza katika mahojiano na gazeti hili, Nkoswe alisema ni jambo ambalo ni jema kwa serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli kuonesha mapema kwamba haina utani dhidi ya vitendo vya rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma.
Nkoswe ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa kwa miongo miwili; 1977 hadi 1987 alijiunga Chadema mwaka 2010 baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM.
“Binafsi nimefurahishwa sana na hatua za serikali hii kwa sababu uozo ambao tumekuwa tukiupigia kelele, si viongozi wa upinzani bali pia wananchi wa kawaida, ni haya ambayo sasa tunayaona na kuyasikia,” alisema Nkoswe.
Aliongeza: “Kazi hii anayoifanya Rais ni ngumu na nzito na kama anavyosema mwenyewe Rais, tumwombee. Tumwombee kwani endapo atafanikiwa katika hili, nchi yetu, mbali na kuwa na maendeleo lakini pia itakuwa ya heshima duniani.”
Alisema ameguswa na kitendo cha makatibu wakuu na manaibu wao kula kiapo cha maadili hadharani akisisitiza kuwa kiapo hicho ni sawa na Azimio la Arusha, lingine lililosifika kwa kusimamia madhubuti maadili ya uongozi.
“Hatua hii ya Rais wetu Magufuli kupambana na kuanika uozo wote naweza kumfananisha na Hayati Edward Sokoine. Pia zinafanana na hatua za mwanzo alizochukua Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere dhidi ya viongozi waliokuwa wakijilimbikizia mali na kuwakoga wananchi mara tu baada ya Uhuru,” alisema.
Hata hivyo, aliitaka serikali kuwaanika hadharani waliohusika na kashfa za Richmond, Meremeta, rada, EPA na zote zilizojiri huko nyuma. Alihimiza Watanzania kujenga tabia ya uwajibikaji kwa kufanya kazi kwa kujituma bila kusubiri kusukumwa, uaminifu na kutanguliza mbele uadilifu.

Tanzania kutimua wageni wasio na vibali

Masauni


Tanzania imeanza rasmi operesheni ya kuwasaka na kuwafurusha raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini humo kinyume cha sheria.
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Hamad Masauni ameambia wanahabari kwamba operesheni hiyo imeanzishwa baada ya kubainika kwamba kuna raia wengi wa kigeni wanaofanya kazi Tanzania kinyume cha sheria.
Operesheni hiyo hiyo inafanyika siku chache baada ya wizara inayohusika na ajira kumuagiza kamishna wa kazi nchini humo kufuta vibali vya kazi vya muda kwa wageni.
"Serikali haiwezi kukaa kimya wakati vijana wanakosa ajira huku kazi zile walizotakiwa kufanya zikifanywa na raia wa kigeni,” Bw Masauni amenukuliwa na gazeti la Mwananchi.
Afisa wa uhamiaji wa mkoa wa Dar es Salaam John Msumile amesema wanatarajia kuwakamata wageni zaidi ya 350.
Kuhusu vibali va kazi vya muda, Bw Masauni amesema serikali itaandaa utaratibu mwingine wa kushughulikia watu wanaotaka kufanya kazi Tanzania kwa muda.
Hii ni baada ya serikali kupokea malalamiko mengi kuhusu suala hilo.
Mwishoni mwa mwaka waziri katika afisi ya waziri mkuu anayehusika na ajira Jenista Mhagama pamoja na naibu waziri Anthony Mavunde walifanya ziara za kushtukiza katika kampuni mbalimbali.
Waligundua raia kadha wa kigeni waliokuwa wakifanya kazi bila vibali halali.

SAMATTA, ULIMWENGU WABEBA TUZO YA KWANZA TP MAZEMBE IKITANGAZWA KIKOSI BORA AFRIKA


Kikosi cha TP Mazembe kimeteuliwa kuwa kikosi bora barani Afrika mwaka 2015 katika tuzo za Mwanasoka Bora Afrika zinazoendelea jijini Abuja nchini Nigeria.

Mazembe ambao ni mabingwa watetezi barani Afrika, wametwaa tuzo hiyo na kuwapiga bao USM Alger ya Algeria ambao waliwafunga katika mechi zote mbili za fainali ubingwa wa Afrika.

Watanzania wawili, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanakipiga katika klabu hiyo ya Lubumbashi, DR Congo.


Katika mechi mbili za fainali, TP Mazembe ilianza kushinda ugenini kwa mabao 2-1, ikarejea nyumbani Lubumbashi na kushinda kwa mabao 2-0.

Katika mechi zote mbili, Mtanzania Samatta alifunga hivyo kuweka rekodi ya kufunga mabao mawili katika mechi mbili za fainali.

Pia katika mechi hizo mbili za fainali, Watanzania hao, Samatta na Ulimwengu, wote walicheza mechi zote mbili, hivyo mchango wao kwa Mazembe kuwa kikosi bora Afrika ni mkubwa sana.

SAMATTA MWANASOKA BORA AFRIKA, KADIABA ASHIKA NAMBA 2,

Image result for BREAKING
 


 


 Mbwana Ally Samatta ndiyo wanasoka bora Afrika kwa wale wanaocheza ndani ya bara hili.
Samatta ameibuka mwanasoka bora kwa kuwashinda Muteba Kadiaba ambaye ni kipa mkongwe wa TP Mazembe na Bounedjah Baghdad wa Algeria anayekipiga Etoile du Sahel.
 
Image result for SAMMATA
 Samatta ametwaa tuzo hiyo kwenye utoaji utoaji tuzo za wachezaji bora zinazoendelea jijini Lagosi Nigeria.
Watanzania wengi walikuwa wakisubiri kwa hamu kufanyika kwa tuzo hizo ili Samatta aweke rekodi barani Afrik

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.