Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » »

Mipango ya Madee 2015 ikoje? Shilole na tattoo nyingine? Harmonize Kachora tatooo ya simba??

Ni January 2016 tarehe zimeanza kusomeka mdogomdogo mtu wangu na mwaka ndio umeanza kihivyo yani !!
Msanii kutoka Tip Top Connection, Madee amesema mbali ya muziki wake mwaka 2016 mpango mkubwa mwingine alionao ni kuanzisha kampuni ya kukodisha magari… Yes yes, mambo yako hivyo na Madee amethibitisha kwamba mzigo unaanza time yoyote soon kuanzia sasahivi !!
MADEE
Madee
Kila la heri kwa Madee na mipango yake, naamini fans wake wake watamuunga mkono pia kwenye biashara yake mpya.
Tulizijua tattoo za Shilole na Nuh Mziwanda baada ya mapenzi yao kukolea !! Mitandaoni kuna story kwamba mambo yameenda tofauti, hakuna mapenzi tena kati yao.. zile tattoo je ?!
Huu ndio muonekano wa tattoo ya Shilole kwa sasa.
Huu ndio muonekano wa tattoo ya Shilole kwa sasa.
Shilole amesema ameibadilisha tattoo ya Nuh na hata likitokea penzi jingine kubwa, masuala ya tattoo ‘NO’… Mapenzi yataenda ila hakuna mambo ya kuchorana tattoo tena !!
Harmonize nae ana tattoo, anawaza itakuwaje siku yeye na Diamond Platnumz wakifikia mwisho wa ushkaji wao ?! Harmonize kasema hata kitokee kitu gani, hayuko tayari kuijutia tattoo hiyo kwa sababu ya msaada mkubwa alioupata kutoka kwa Diamond.
HARMONIZE
Tattoo ya Harmonize
Stori zote na kama unataka kuwasikiliza mastaa hao watatu kwenye majibu yao unaweza kubonyeza play kwenye hii sauti mtu wangu.
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.