Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » »

WAZIRI KITWANGA ATEMBELEA UHAMIAJI, ATANGAZA OPERESHENI YA KUKAMATA WAHAMIAJI HARAMU NCHINI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Katika ziara hiyo, Waziri Kitwanga aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji kuanz rasmi kwa operesheni ya kuwakamata Wahamiaji Haramu nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai) akiwasalimia wananchi wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kikazi katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Katika hotuba yake, licha ya maelekezo mengine aliyoyatoa kwa viongozi wakuu, pia aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji kuanza rasmi kwa operesheni ya kuwakamata Wahamiaji Haramu nchini.
Afisa Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa Hati za Kusafiria, Amir Hassan (kushoto), akitoa maelezo ya jinsi wanavyozichapisha Hati za Kusafiria, kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) ambaye alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, wakati Waziri huyo alipokuwa anafanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwaeleza jambo Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, John Mngodo, na wapili kulia (waliokaa) ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile na kulia ni Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wasita kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Wasita kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NSSF KUKABIDHI DARAJA LA KIGAMBONI JANUARI 2016

Waziri Ofiisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau wakati ziara yake Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau akifafanua jambo.
 Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza wakati alipofanya ziara katika Daraja la Kigamboni.
 Sehemu ya Daraja la Kigamboni.
 Waziri akipata maelezo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
 Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi John Msemo akimuonesha Waziri muunganiko wa barabara zinazoingia katika  daraja hilo. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Waziri Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni wakati waziri huyo  alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, ambapo ujenzi wake utakamilika mwishoni mwa mwezi Januari mwakani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau (katikati) wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mradi ujenzi wa Daraja hilo. Mhandisi Kareem Mataka. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau (wa pili kulia), akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia), alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, ambalo ujenzi wake utakamilika Januari Mwakani. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo ujenzi wake utakamilika Januari Mwakani. 

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama amelitaka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuhakikisha linakabidhi daraja la Kigamboni ifikapo Januari, 2016.

Pia ametoa fursa kwa shirika hilo na mengine nchini kama yataweza kuja na mradi wa ujenzi wa daraja kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar.

Hayo alibainisha jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa daraja hilo, ambalo linatarajiwa kukamilika mwakani.

Alisema ujenzi wa daraja hilo, umegharimu kiasi cha Dola za Marekani 143.5, ambapo serikali imetoa asilimia 40, huku NSSF ikitoa asilimia 60 ya fedha zote.
“Tunaliomba shirika hili, lihakikishe linaheshimu nha kuzingatia muda uliotoa katika kukabidhi daraja hilo mwakani licha ya kujitokeza ujenzi mwingine wa barabara ya Kilomita moja,”alisema.
Alisema shirika hilo linapaswa kulikabidhi daraja ifikapo Januari 30 au kabla ya muda huo, kwani ukamilifu wake utapunguza adha ya foleni na kukuza sekta ya uchumi inayotarajiwa kukuwa kwa kasi.

Katika hatua nyingine, Mhagama alisema endapo mradi ukiwa katika ubora na viwango vinavyotakiwa utadumu kwa muda mrefu na kuisaidia Seriali katika kukuza uchumi.
“Miradi ya namna itasaisdia kukuza uchumi wa ndani na nje ya nchi, pia inatufundisha kujifunza ili kujua kwamba tunaweza kuhimili miradi mingine mikubwa zaidi ya huu,”alisema.
Kuhusu daraja la kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar, alisema uwezekano wa kujengwa upo endapo mashirika yakijitokeza na mradi huo. “Kila kitu kinawezekana, hivyo kama Shirika litajitokeza serikali ipo tayari kwa kila kitu kuunga mkono mkakati watakao kuja nao,”alisema.
Naye Mkurungenzi wa NNSF, Dk.Ramadhan Dau alisema ujenzi wa daraja hilo umekuwa wa kasi licha ya matatizo yaliyojitokeza, hivyo Watanzania watarajie Januari  mwakani kulitumia.
“Bado kuna sehemu nyingine ambazo tutamalizia ila hadi Januari litakuwa limekamilika kwa asilimia 100, hivyo tunaipongeza serikali kwa ushirikiano uliotuonyesha,”alisema.
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.