Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » » Wanasiasa waonywa kuingilia kazi za NEC

Wanasiasa waonywa kuingilia kazi za NEC

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka viongozi wa vyama vya siasa na serikali kuitoingilia mchakato wa kusimamia na kuendesha uchaguzi, bali wawaache maofisa wa Tume hiyo kufanya kazi yao.
Tahadhari hiyo imetolewa ikiwa zimebaki siku chache kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika majimbo ya Arusha Mjini mkoani Arusha na Handeni mkoani Tanga. Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Damian Lubuva aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu upigaji kura katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Jumapili wiki hii kwenye majimbo hayo.
Aidha, uchaguzi huo pia utafanyika katika kata tatu za Ipala Halmashauri ya Dodoma, Nyamilolelwa katika Halmashauri ya Geita na Mvomero katika Halmashauri ya Mvomero.
“Viongozi wote wa serikali na vyama vya siasa pamoja na umuhimu wa majukumu yao wasiingilie mchakato wa kusimamia na kuendesha uchaguzi, maofisa wa Tume waachwe wafanye kazi zao bila kuingiliwa,” alisema Jaji Lubuva.
Lubuva alisema utaratibu utakaotumika katika uchaguzi huo ni ule ule ambao ulitumika katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu hivyo kila mmoja ahakikishe anafuata sheria za uchaguzi.
Alisema mawakala wa vyama vya siasa wanaruhusiwa kuwepo vituoni, lakini watakaokuwa hawana barua hawataruhusiwa kuingia katika vituo vya kupigia, kuhesabia na kujumlishia kura.
“Sheria zitakazotumika katika uchaguzi huu ni zile zile zilizotumika katika uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu. Vituo vitafunguliwa kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni na kila mmoja abebe kadi yake ya kupigia kura,” alisema na kuongeza kuwa Tume inaamini hali ya amani na utulivu ambayo imekuwepo kabla ya na baada ya uchaguzi itaendelea kudumishwa ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani kwa ustawi wa taifa zima.
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.