Serikali ya Tanzania imefanya maamuzi ya kumsimamisha mwingine December 23
December 23 2015 imenifikia taarifa ya
maamuzi yaliyoamriwa na Serikali ya Tanzania ambapo Mtendaji Mkuu wa
Mradi wa Mabasi ya mwendokasi DART, Bi. Asteria Mlambo amesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
Tuhuma zilizotajwa kusababisha
kusimamishwa kwa Mkurugenzi huyo ni ishu ya kukiukwa kwa kanuni za
kumtafuta mtoa huduma wa mpito wa huduma za mabasi ya mwendokasi.
Katika kukiukwa kwa kanuni hizo,
Serikali imesema kuna watumishi ambao watachunguzwa na kuchukuliwa hatua
kwa kushindwa kumshauri vizuri Mtendaji Mkuu huyo.
Taarifa hiyo kutoka kwa Waziri George Simbachawene hii hapa..
0 comments:
Post a Comment