Mwandishi wa nyimbo za Rihanna asema Travi$ Scott ndio anachelewesha album ya ANTI kutoka.
Glass John ameweka wazi kuwa boy friend wa Rihanna Travi$ Scott anachelewesha album mpya ya Rihanna Anti kutoka.
Glass John ambaye aliwahi kufanya kazi na Chris Brown na Rihanna
ametumia twitter kusema kuwa anajaribu kumshawishi Jay Z atoe album hii
ila Travi$ Scott amekuwa akimshauri Rihanna asitoe album hii mpaka
mashabiki waonyeshe kuitaka zaidi.Glass John anasema kuwa wimbo kama “Kiss It Better” anataka utoke ila Travis Scott ndiye alimshauri Rihanna atoe “Bitch Better Have My Money,”.
Mwandishi huyu pia ameponda kitendo cha Travi$ Scott kumpeleka Rihanna kwenye club za mitaani ambazo huwa na fuji na kufyatuliana risasi.
0 comments:
Post a Comment