Hii ndio Top 10 ya wachezaji soka maarufu katika mtandao wa Instagram duniani …
Mtandao wa kijamii wa Instagram
umeanzishwa miaka mitano iliyopita ila toka kuanzishwa kwake unatajwa
kuwa miongoni mwa mitandao ya kijamii inayokuwa kwa kasi zaidi duniani,
huu ndio mtandao ambao maarufu kwa watu kupost picha na video zao.
December 10 mtu wangu naomba nikusogezee Top 10 ya mastaa maarufu zaidi
katika mtandao wa Instagram yaani wanafollowers wengi.
Cristiano Ronaldo
ambaye ni mkali wa kuvunja rekodi za soka kwa sasa ndio staa wa soka
anayetajwa kuwa na wafuasi wengi katika mitandao yote ya kijamii. Huenda
ukawa unashangazwa na list ya wachezaji wa America kuwa wengi katika list hii, ukweli ni kwamba America
mtandao wa Instagram unatajwa kuwa na watumiaji milioni 400 na milioni
39.5 kati ya hao wamewafollow wachezaji soka wakubwa. Hii ndio Top 10
mtu wangu.
10- Thiago Silva wa klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa (PSG) ana followers milioni 8
9- Karim Benzema wa klabu ya Real Madrid ya Hispania na timu ya taifa ya Ufaransa ana followers milioni 8.3
8-Ronaldinho ambaye aliwahi kuchezea timu ya taifa ya Brazil ila kwa sasa hana timu ana jumla ya followers milioni 8.7 .
7- Zlatan Ibrahimovic mshambuliaji wa klabu ya PSG ya Ufaransa na timu ya taifa ya Sweden ana followers milioni 10.
6- David Luiz listi hii wachezaji wa Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa wametawala, yeye ana followers milioni 11.
5- Gareth Bale ni mchezaji anayeshikilia rekodi ya usajili ya Dunia anaitumikia klabu ya Real Madrid ya Hispania na timu ya taifa ya Wales ana jumla ya followers milioni 11.4
4- James Rodriguez anakipiga katika klabu ya Real Madrid anatajwa kufikia followers milioni 16.7
3- Lionel Messi wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina anatajwa kuwa na followers milioni 30.5
2- Neymar ndio mchezaji wa pili wa FC Barcelona kuwa katika hii list ana followers milioni 36.5
1- Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ndio anatajwa kuwa staa maarufu zaidi katika mitandao ya kijamii ikiwemo instagram ana followers milioni 39.4
0 comments:
Post a Comment