Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » »

Hii ndio idadi ya followers wa Vanessa Mdee Instagram… kawagusa Diamond & Wema Sepetu!

Najua nina watu wangu ambao ni mashabiki wakubwa wa staa kutoka bongo flevani, Vanessa Mdee a.k.a Vee Money. Najua pia mmekuwa mkimfuatilia Vanessa kwenye matukio yake mengi na kwa ajili ya upendo wenu mmeamua pia kuwa karibu naye kwenye Instagram ili chochote atakachokifanya kisikupite.
vee6
Ukitembelea Instagram page ya Vee Money @VanessaMdee sasa hivi utakutana na mabadiliko kwenye idadi yake ya followers… staa huyo wa muziki wa Bongo Fleva anaingia kwenye list kama staa wa pili wa muziki kufikisha idadi kubwa ya followers kwenye Instagram… na ukitembelea page yake sasa hivi hii ndio latest number ya followers wa Vanessa Mdee 1MILLION!
vee1
Kwa upande wa muziki alianza Diamond Platnumz ambaye kwa sasa anashikilia followers milion 1.4 kwenye Instagram huku Vanessa Mdee akiendeleza list kwa wasanii wa muziki.
vee2
Mastaa wengine ambao wenyewe hawajihusishi na muziki lakini wameweza kugonga idadi kubwa ya followers kwa Tanzania ni pamoja na hawa watu wetu…
Wema Sepetu actress wa Bongo Movie ambaye kwa sasa anashikilia followers 1.1 Million.
vee3
Mafanyabiashara na mwanamitindo, Jokate Mwegelo pia ni miongoni ya mastaa wachache kutoka Tanzania kushikilia watu milion 1 kwenye page yake ya Instagram.
vee7
Akifuatiwa na mtangazaji kutoka Clouds Fm , Millard Ayo na yeye akiwa anashikilia idadi wa watu 1.1 milion followers kwenye Instagram.
vee4
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.