Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » »

Adele anafunga mwaka wa 2015 na haya mambo sita: Umaarufu, Album mpya na mengine!

Adele ndiye staa wa muziki anayefunga mwaka wa 2015 kwenye headlines za burudani Marekani na dunia nzima akiwa ameuza zaidi ya nakala milion 5 za single yake mpya ‘Hello’ huku video yake ikiwa imegusa watazamaji milion 700 kwenye mtandao wa YouTUBE! Ujio mpya wa Adele kwenye kurasa za burudani umepokelewa kwa muamko mkubwa sana duniani.
TIME4
Nimekutana na interview ya Adele na jarida la TIME Magazine la Marekani na ndani yake staa huyo amegusia vitu vingi ikiwemo album yake mpya 25, social media pamoja na mauzo ya juu nchini Marekani.
TIME2
Hivi ni baadhi ya vitu alivyovigusia Adele na interview yake na TIME Magazine:
Mauzo ya nakala zaidi ya mamilioni Marekani: Inashangaza kidogo na kunishitua sana. Ukizingatia mimi hata sio Mmarekani. Labda wanafikiri nina undugu na Malkia…
TIME
Mtazamo wake kuhusu kuitwa ‘Brand’: Kila mtu analitumia neno hilo. Sipendi kuitwa ‘brand’ wananifanya nionekane kama aina fulani ya bidhaa au kama packet la kripsi… msanii ni package ya vitu vingi!
SATURDAY NIGHT LIVE -- "Matthew McConaughey" Episode 1689 -- Pictured: Musical guest Adele performs on November 21, 2015 -- (Photo by: Dana Edelson/NBC/NBCU Photo Bank via Getty Images)
Kwanini watu huupokea vizuri muziki wake: Uhalisia nilionao ni kwamba sioni aibu kuimba ukweli unaonigusa hata kama mimi ndio mwenye makosa. Kila mtu hufanya makosa. Watu wengi hujifanya wajasiri kwasababu wanaogopa kuonyesha udhaifu wao. Mimi najaribu kuimba nyimbo zinazogusa vitu vya ukweli kwa mashabiki wangu kwa  sababu kama mimi hata wao wanaumizwa na vitu mbalimali maishani japo natumaini pia nyimbo zangu zitaleta furaha kwenye maisha ya mashabiki wangu na sio huzuni na machungu“.
TIME7
Mitandao ya kijamii ina nafasi gani kwake: Napenda kuweka mambo yangu private… kuwa na privacy inakuwezesha kuandika nyimbo za ukweli utakaogusa watu, waupende au wasiupende bado utakuwa ukweli. Maisha yangu yamebadilika sana toka niachie ‘Hello’ na hiyo inanipa changamoto, hivyo siwezi kukaa kusubiria likes milioni na kwa picha moja… nitapata wapi muda wa kutunga nyimbo zitakazogusa watu? Huo sio uhalisia“.
TIME6
Maisha yake binafsi ya nyumbani yapoje: Nina maisha ya kawaida, nahisi watu wengi wangekuwa wanajua jinsi ambavyo maisha yangu ni ya kawaida wangeshangaa. Kama sina kazi zozote huwa nashinda tu nyumbani na familia yangu… ni muhimu kutokupagawa na hivi vitu, ni muhimu pia kukumbuka kuishi kama watu wengine wote wa kawaida.
TIME8
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.