Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » »

Achana na headlines za Steve Harvey za Miss Universe, kutana na list ya mastaa kumi wa soka waliowahi kudata kwa mamiss …Najua headlines za Mashindano ya Miss Universe zimemalizika wiki hii, licha ya kuwa MC  wa sherehe hiyo Steve Harvey kumtangaza kimamkosa Miss Colombia Ariadna Gutierrez Arevalo kama mshindi ila baadae alisahisha kosa hilo, mtu wangu wa nguvu December 24 naomba nikusogezee mastaa kumi wa soka waliowahi kudata kwa mamiss.
10- George Best na Mary Stavin
Staa wa zamani wa klabu ya Man United George Best aliwahi kuwa katika mahusiano na mrembo kutoka Sweden Mary Stavin aliyewahi kushinda taji la Miss World 1977. Mahusiano ambayo yalidumu kwa miaka mitatu, George Best amewahi kuandika katika kitabu cha historia yake kuwa amewahi kuwa na mahusiano na mamiss saba.
George Best and Mary Stavin 14535JP
George Best na Mary Stavin
9- Mikel Arteta na Lorena Bernal
Lorena Bernal ambaye ameolewa na nahodha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta toka mwaka 2010, ni muigizaji, mwanamitindo na amewahi kushinda taji la Miss Spain akiwa na umri wa miaka 17 ilikuwa mwaka 1999, lakini mrembo huyo kutokana na umri wake kuwa mdogo hakushirili Miss World.
Mikel-Arteta-and-Lorena-Bernal
Mikel Arteta na Lorena Bernal
8- Tomas Rosicky na Radka Kocurova
Radka Kocurova aliwahi kushiriki kuwania taji la Miss Czech Republic mwaka 2002 lakini hakufanikiwa kushinda na mwaka 2014 aliolewa na Tomas Rosicky mkali ambaye anaichezea klabu ya Arsenal.
Tomas-Rosicky-and-Radka-Kocurova
Tomas Rosicky na Radka Kocurova
7- Jamie O’Hara na Danielle Lloyd
Kiungo wa klabu ya Fulham amewahi kuwa katika mahusiano na mwanamitindo na aliyekuwa Miss wa zamani wa Uingereza Danielle Lloyd tangu mwaka 2009 na walifanikiwa kupata watoto wawili, kabla ya kuamua kuachana mwaka uliopita.
Jamie-OHara-And-Danielle-Lloyd
Jamie O’Hara na Danielle Lloyd
6- Jermain Defoe na  Imogen Thomas
Mshambuliaji wa Sunderland Jermain Defoe ametajwa kuwa na tabia ya kupenda kutoka na warembo, amewahi kutoka na warembo kadhaa ikiwemo Miss Wales mwaka 2003 Imogen ThomasDanielle Lloyd aliyekuwa Miss Uingereza mwaka 2004.
Imogen-Thomas-2
Jermain Defoe na Imogen Thomas
5- Gianluigi Buffon na Alena Seredova
Alena alishinda taji la Miss Czech Republic mwaka 1998 na kwenda kushiriki Miss World alipoambulia kushika nafasi ya nne mwaka 1998, Alena alikuwa katika mahusiano na kipa wa Juventus Gianluigi Buffon toka mwaka 2005 na mwaka 2011 walifunga ndoa na kuachana mwaka 2014.
Gianluigi-Buffon-and-Alena-Seredova
Gianluigi Buffon na Alena Seredova
4- Alessandro Costacurta na Martina Colombari
Colombari alishinda taji la Miss Italia mwaka 1991 akiwa na umri wa miaka 16, ni muigizaji, mwanamitindo na mtangazaji wa TV , aliolewa na mchezaji wa zamani wa AC Milan Alessandro Costacurta mwaka na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume.
Alessandro-Costacurta-And-Martina-Colombari
Alessandro Costacurta na Martina Colombari
3- Davide Bombardini na Giorgia Palmas
Palmas ambaye alikuwa mshiriki wa Miss World mwaka 2000 na kushindwa na Miss kutokea India, alichumbiwa na mkali wa soka  Davide Bombardini mwaka 2004 na kufanikiwa kupata mtoto wa kike, lakini mahusiano yao yalivunjika mwaka 2011.
Davide-Bombardini-and-Giorgia-Palmas
Davide Bombardini na Giorgia-Palmas
2- Gylfi Sigurdsson na Alecandrea Ivarsdottir
Alecandrea Ivarsdottir aliyeshinda taji la Miss Iceland mwaka 2008 na kufika nusu fainali ya Miss World mwaka huo, amekuwa katika mahusiano na Sigurdsson toka wamekutana mwaka 2010 katika michuano ya Kombe la Dunia.
Gylfi-Sigurdsson-and-Alecandrea-Ivarsdottir
Gylfi Sigurdsson na Alecandrea Ivarsdottir
1- Ivica Mornar na Fani Capalija
Capalija alikuwa mshiriki wa Miss Croatia, Miss Europe na Miss World mwanzoni mwa miaka 1990, kabla ya kuolewa na mchezaji wa zamani wa Sevilla na Portsmouth Ivica Mornar na kuachana mwaka 2004.
Ivica-Mornar-and-Fani-Capalija
Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.