IRINGA
Serikali imetakiwa
kusimamia sheria ya mizani na vipimo ya mwaka 1982kwa umakini ili wakulima na wafanyabiashara waweze
kunufaika na kilimo.
Ushauri huo umetolewa
na mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara mkoani Iringa TCCIA Bw Lukas
Mwakabungu wakatika akiongea na kituo hiki.
Bw Mwakabungu amesema
ili usimamizi huo ufanyike kwa ufanisi ni vyema viongozi wote wakawajibia
kuanzia katika ngazi ya juu ya uongozi
wakiwemo wakuu wa mikoa.
Aidha mwakabungu
amesema halmashauri za wilaya zinatakiwa kuunda sheria ndogondogo zitakazo
wabana wakiukaji wa sheria ya mizani na vipimo ya mwaka 1982.
Hata hivyo amewataka
wafanyabiashara kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za nchi na kutokukwepa
kulipa kodi kwani kukwepa kulipa kodi ni kuikosesha serikali kupata mapato yake
halisi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment