Miaka
19 iliyopita siku kama ya leo meli ya Mv Bukoba ilipinduka na kuzama
katika ziwa Victoria ikiwa takribani umbali wa kilometa 10 kabla ya
kutia nanga bandari ya Mwanza.
Inakadiriwa watu zaidi ya 800 walipoteza maisha katika mkasa huo. Meli hiyo iliyokuwa na uwezo wa kubeba watu 500 inakadiriwa watu zaidi ya 1000 walikuwa wameabiri katika meli siku hiyo ya tukio kutokea bandari ya Kemondo, Kagera kuelekea jijini Mwanza.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu azilaze mahala pema roho za wote walifariki kutokana na mkasa huo.
0 comments:
Post a Comment