Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » » Vyombo vya habari vitumike katika kutangaza utalii wa kiutamaduni

Vyombo vya habari vitumike katika kutangaza utalii wa kiutamaduni








IRINGA:
Vyombo vya habari mkoani hapa vimetakiwa kutangaza vivutio vya utalii wa kiutamaduni vilivyopo mikoa ya nyanda za juu kusini ili kuongeza idadi ya watalii na kukuza pato la taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari wa mkoani hapa meneja msaidizi wa mradi wa fahari yetu Bw Jimsoni Sanga amesema vombo vya habari vitumike katika kutoa elimu ya utunzaji wa utamaduni kwa maendeleo endelevu ya utalii.

Amesema takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kupanda kwa idadi ya watalii kwa mikoa ya nyanda za juu kusini ukilinganisha na miaka 5 iliyopita.

Vilevile amewataka wamiliki wa hotel na nyumba za kulala wageni kutoa huduma kwa kiwango kizuri ili kuvutia watalii kuja kutembelea vivutio vilivyopo mikoa ya nyanda za juu kusini.
MWISHO




Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.