Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » » POLISI WATAKIWA KUTOWABUGUDHI WANANCHI WAKATI WA DORIA

POLISI WATAKIWA KUTOWABUGUDHI WANANCHI WAKATI WA DORIA





Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha MrakibuwaPolisi (SP) Jumanne Muliro amevitaka vikundi vya ulinzi shirikishi pindi wanapokuwa katika kazi za doria kutowabughudhi wananchi badala yake wanatakiwa kufanya kazi zao kwa kufuata sheria.

Amesema utendaji bora wa kazi kwa kuzingatia nidhamu na sheria utaongeza imani kwa wananchi hali ambayo itawafanya wajitolee na kuendelea kuvichangia vikundi hivyo hatimaye kuboresha maslahi yao wenyewe na vikundi hivyo kwa ujumla kwa maana ya vifaa.

Amesema hakuna sheria inayomkataza mtu yoyote kutembea usiku lakini pia ni jukumu la askari kumhoji yeyote mtakayekutana naye usiku kwa kutumia taaluma walionayo ili kuweza kubaini ukweli.

Ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa vikundi viwili vya Ulinzi Shirikishi uliofanyika katika kata ya Moshono ambapo jumla ya askari 50 wa vikundi hivyo walihudhuria.

Amesema ili kazi zao ziende vizuri na kuendelea kujenga imani kwa wananchi wanatakiwa wanapoingia kazini wasiwe wamelewa hali ambayo itaendelea kuleta uelewa na masikilizano baina ya wanaohoji na wanaohojiwa na kuepusha matukio ya kutojichukulia sheria mkononi.

Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.