Country Fm Iringa 88.5 Iringa,91.1 Mbeya
Home » » Marekani tayari kuzungumza na Assad

Marekani tayari kuzungumza na Assad

Marekani imesema italazimika kufanya mazungumzo na Rais wa Syria Bashar al Assad ili kuvimaliza vita vya Syria ambavyo vimeingia mwaka wake wa tano hapo jana.

Zaidi ya watu laki mbili wameuawa katika vita hivyo huku kiasi ya nusu ya idadi ya raia wa nchi hiyo wakiachwa bila ya makaazi katika mzozo ambao makundi ya kutetea haki za binadamu yameishutumu jumuiya ya kimataifa kwa kuwatelekeza watu wa Syria.


Baada ya miaka minne ya kusisitiza Assad sharti aondoke madarakani, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amekiri kuwa Marekani haina budi bali kushauriana na Assad ili vita hivyo kukoma.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CBS, Kerry amesema nchi yake imekuwa ikitaka kufanya mazungumzo na kiongozi huyo kwa misingi ya makubaliano yaliyofikiwa Geneva ya kutafuta amani Syria na kuongeza atashauriana na washirika wake ili kupatikane suluhisho la kidiplomasia.

Ahsante kwa maoni yako,endelea kusikiliza redio country fm Iringa-One community
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

SIKILIZA COUNTRY FM

Pages

Pages

radio country fm,one community. Powered by Blogger.